Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
JUMUIYA ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Kibaha
Mjini, kwa kushirikiana na makatibu 11 wa kata zote wilayani hapa,
wameandaa mpango mkakati wa kuimarisha uhai wa jumuiya hiyo, ili iweze
kutekeleza majukumu yake ya kila siku.
Katibu wa UVCCM wilayani hapa, Khalid King, alisema lengo ni kuongeza
wanachama wapya kwa kila kata na kuvuna wanachama 1,000 hadi
itakapofika mwishoni mwa mwezi huu.
Alisema katika mkakati huo hadi sasa wameshapata wanachama wapya 400
kwa kipindi cha miezi mitatu na wanatarajia kupata zaidi ya wanachama
1,000 ndani ya mwezi huu.
King alitaja mpango mwingine ni kuunganisha vijana bila kujali
itikadi za kisiasa ikiwemo wajasiriamali, madereva wa piki[iki
‘bodaboda’ kwa kutumia michezo na kuwaweka katika makundi, ili waweze
kukopesheka.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment