Home » » TAARIFA :WAZIRI WA ELIMU SHUKURU KAWAMBWA HAJAFARIKI YUPO NCHINI CANADA KIKAZI.

TAARIFA :WAZIRI WA ELIMU SHUKURU KAWAMBWA HAJAFARIKI YUPO NCHINI CANADA KIKAZI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


TAARIFA TOKA BAGAMOYO

Ndg Watanzania,WanaBagamoyo na wapenda maendeleo, kwa niaba ya CCM-Bagamoyo na Ofisi ya Mbunge-Jimbo la Bagamoyo napenda kuleta kwenu Masikitiko yetu kwa niaba ya Chama na Familia ya Mheshimiwa Mbunge Shukuru Jumanne Kawambwa kutokana na Usumbufu ambao umesababishwa na habari zinazoenezwa Mitandaoni kwamba Mheshimiwa Kawambwa amekumbwa na Umauti akiwa njiani anaelekea Mwanza.




UKWELI
Mheshimiwa Shukuru Jumanne Kawambwa yupo Nchini Canada Akitimiza majukumu yake. Hivyo Watanzania na wana Bagamoyo mnaombwa radhi kwa usumbufu uliotokea na kwamba Mheshimiwa Mbunge yuko na Afya njema na utekelezaji wa Majukumu unaendelea kama kawaida.

Ndg.Ridhiwani Kikwete (Mnec)
Mbunge -Chalinze

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa