Timu ya kikosi cha waandaaji wa Kipindi cha Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula wakiwa katika Picha ya Pamoja kabla ya Mechi kuanza dhidi ya Vijana wa Maisha Plus/ Mama Shujaa wa chakula
Baadhi ya Mashabiki wa Timu ya Waandaaji wa Kipindi cha Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula wakiwa wanashauriana na Kufuatilia mtenange kwa umakini zaidi.
Mtenange ukiwa unaendelea
Mashabiki wa timu ya Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula wakiwa wanashangilia Ushindi wao baada ya kuwachabanga Magoli mawili kwa moja timu ya Waandaaji wa kipindi hicho cha Maisha Plus Mama Shujaa wa Chakula mechi iliyochezwa katika Kijiji cha Maisha Plus.
******
Kulikuwa na mambo mengi sana katika Kijiji cha Maisha Plus ambapo walipata Ugeni Mkubwa wakawa na michezo mingi lakini Furaha iliendelea kufana
zaidi pale timu ya mpira wa miguu ya kijiji cha Maisha Plus ilipopata ushindi
wa mabao 2–1 dhidi ya wafayakazi na waandaaji wa kipindi cha Maisha Plus na
Mama Shujaa wa Chakula 2014. Magoli yote yalifungwa katika kipindi cha kwanza
huku timu ya wafanyakazi ikiongoza kwa goli moja huku timu ya kijiji cha Maisha
Plus kusawazisha na baadaye kuongoza kwa goli moja na kuwa washindi. Kwa upande
wa wafanyakazi goli lilifungwa na Erick Mlindima huku timu ya kijiji goli la
kusawazisha lilifungwa na Boniphace Meng’anyi mwenye namba ya ushiriki MP 06
huku goli la ushindi lilifungwa na Said Rashid mwenye namba ya ushiriki MP 29.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment