Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KINA mama nchini wametakiwa kuachana na tabia ya kuwa tegemezi na
badala yake wajiunge katika vikundi vya ujasiriamali kwa lengo la
kupamabana na umasikini.
Rai hiyo ilitolewa mjini hapa jana na mjumbe wa Kamati ya Uekelezaji
ya Umoja wa Wanawake Wilaya ya Kibaha kupitia CCM, Elina Mgonja wakati
wa ziara ya UWT ya kuwatembelea kina mama hao kwa lengo la kubaini
changamoto zinazowakabili.
Mgonja alisema kwamba kwa sasa kina mama wanatakiwa kuwa na mtazamo
chanya wa kuelekeza nguvu zao kushiriki kufanya kazi, hali ambayo
itaweza kuwaletea mabadiliko makubwa.
“Wanawake inabidi kuwa na mshikamano wa hali ya juu katika
kushirikiana katika majukumu mbalimbali, na kikubwa kujiunga katika
vikundi vya ujasiriamali ambavyo nina imani vitakuwa mkombozi kwenu,”
alisema.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Kibaha, Mwanaidi Kiongoli,
aliwataka kina mama hao kutokuwa waoga katika kufanya uamuzi, kwani
kufanya hivyo wanajirudisha nyuma.
Chanzo;anzania Daima
0 comments:
Post a Comment