Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wakizungumza katika mkutano wa kampeni wa mgombea ubunge kwa tiketi
ya CCM, Ridhiwani Kikwete, wakazi hao walisema adha hiyo imekuwa
ikisababisha wakati mwingine kushindwa kufanya shughuli za maendeleo.
Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho, Ridhiwani, aliwaomba wananchi hao kumchagua ili ashughulikie kero hiyo.
Ridhiwani aliahidi endapo atachaguliwa kuwa mbunge atajenga visima viwili vya pampu ili kutatua changamoto hiyo.
Katika hatua nyingine, Ridhiwani aliahidi kumsomesha kijana Abdala
Salehe, mkazi wa Kijiji cha Tonga kuendelea na masomo endapo
watamchangua kuwa mbunge.
Abdala alifaulu katika Shule ya Sekondari Bagamoyo, lakini ameshindwa kuendelea na masomo kutokana na kukosa watu wa kumsaidia.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment