Home » » Tasaf yapunguza tatizo la mimba

Tasaf yapunguza tatizo la mimba

Ni kwa asilimia 90 wilayani Bagamoyo, baada ya kuanzisha mpango wa kugawa fedha kwa a maskini.
Bagamoyo. 
Zaidi ya asilimia 90 ya wanafunzi wanaopata mimba katika Shule za Msingi na  Sekondari wilayani hapa Mkoa wa Pwani, imepungua kufuatia Mfuko wa  Maendeleo ya Jamii (Tasaf) kutoa pesa kwa kaya maskini.
Mfuko huo wa maendeleo ambao upo katika awamu ya tatu ya utekelezaji wake, imekuwa ikisaidia kaya maskini katika mpango wao wa uhawilishaji fedha ambapo kaya hizo hugaiwa fedha kila mwezi kwa ajili ya kupunguza umaskini.
Tatizo la mimba na utoro wilayani humo pamoja na mambo mengine limeelezwa kuchangiwa na wazazi wengi kutokuwa na kipato cha uhakika hivyo kushindwa kuwapatia watoto wao mahitaji muhimu na kujikuta wakitumbukia katika vitendo viovu ikiwamo matumizi ya dawa za kulevya na mimba.
Mwenyekiti wa Kijiji Fukayosi, Salum Mkecha alibainisha hayo wakati Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi alipotembelea miradi inayofadhiliwa na Tasaf wilayani humo.
Kwa mujibu wa Mkecha, tatizo la mimba limepungua tangu mradi huo umeanza na kwamba mpaka sasa hajapokea taarifa hata moja ya ujauzito kutokana na wananchi kupata mahitaji ya msingi jambo alilodai linachangia hata wananchi hao kupata huduma za afya pindi wanapougua.
Alisema wanafuzi wengi walikuwa wakipata mimba kwa kukosa mahitaji ya msingi na kujikuta wakishindwa kuendelea na masomo huku wavulana wakijitumbukiza katika vitendo viovu kama matumizi ya dawa za kulevya lakini sasa hali ni tofauti.
Mkuu wa Wilaya hiyo Ahmed  Kipozi aliwataka wananchi hao kuzitumia kwa manufaa yao fedha hizo ikiwamo kujiunga na huduma za msingi kama bima ya afya. maendeleo,”alisisitiza Kipozi.
ChanzoMwananchi



0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa