UTARATIBU WA KUTOA LESENI YA BIASHARA.
Ili Mfanyabiashara aweze kupata Leseni ya Biashara, lazima aombe kwa Mamlaka husika:-
Wizara ya Viwanda na Biashara kwa leseni za kundi “A” na Halmashauri
kwa leseni za kundi B. Fomu ya maombi ya leseni za Biashara TFN Na. 211
ya 2004 imeonesha vizuri makundi haya. Mfanyabiashara anatakiwa kutimiza
masharti yafuatayo:-
i. Kujaza fomu ya maombi ya Leseni za Biashara (fomu inapatikana
katika tovuti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa (www.pwani.go.tz) au fika ofisi
za Biashara za Halmashauri za Wilaya za Bagamoyo, Kibaha Wilaya , Kibaha
Mji, Kisarawe, Mkuranga, Mafia, Rufiji, Chalinze na Kibiti.
ii. Ambatanisha nyaraka kama inavyojieleza katika fomu ya maombi (TFN
211 ya 2004) na kuwasilisha Wizarani/ Halmashauri kwa ajili ya ukaguzi
(assessment) na kujulishwa kiasi cha ada cha kulipia;
iii. Kwa Biashara za A, fanya malipo kwenye Benki utakayoelekezwa na Wizara ya Viwanda na Biashara
iv. Kwa Biashara za kundi B fanya malipo kwenye Benki utakayoelekezwa na Halmashauri husika;
v. Wasilisha “pay in slip’ ya Benki na kufuata maelekezo mengine
utakayopewa na Mamlaka ya leseni husika,ili kupata risiti halali ya
Serikali;
Mkoa unawashauri Wananchi wote na hasa wafanyabiashara kuwa hakuna
urasimu wowote wa upatikanaji wa leseni za Biashara.Leseni za Biashara
hutolewa kwa muda wa siku moja, endapo nyaraka zote zimekamilishwa na
mwombaji.
Mwombaji anatakiwa kuwasilisha nyaraka zifuatazo zikiambatanishwa na Ombi Lake:
a. Nakala ya kuandikisha hati ya jina la Biashara au kampuni (photocopy of certificate of incorporation & Extract);
b. “Memorandum, and Articles of Association” ambazo zitaonyesha kuwa
kampuni imeruhusiwa kisheria kufanya biashara inayoombwa, pamoja na
majina ya wamiliki wa kampuni, hisa zao na utaifa wao.
c. Uthibitisho wa uraia kwa kuwasilisha, nakala ya hati ya kusafiria
nje ya Nchi ya Tanzania au hati ya kusafiria katika nchi za Afrika
Mashariki, cheti cha kuzaliwa au hati ya kiapo(Affidavit) kuonyesha kuwa
ni Mtanzania, na kama mgeni ataleta hati ya kuishi nchini daraja la
kwanza (Residence permit class A);
d. Endapo wenye hisa wote wapo nje ya Nchi itabidi maombi yaambatane
na hati ya kiwakili (Power of Attorney) ya kumpa Mamlaka raia wa
Tanzania, raia wa kigeni mwenye hati ya kuishi nchini daraja “A” au hati
ya kufanya kazi nchini daraja “B” inazoainisha kuwa anasimamia kampuni
husika.
e. Nakala ya usha hidi wa maandishi kuwa ana mahali pa kufanyia
biashara (lease agreement, Title deed, Certificate of Occupancy, e.t.c)
f. Hati ya kujiandikisha kama mlipa kodi (Tax payer Identification Number – TIN).
Chanzo Tovuti ya Mkoa wa Pwani
0 comments:
Post a Comment