Na Mathias Canal
Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu leo
Septemba 10, 2017 amefanya kikao na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio
Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani ili kuwaeleza dhamira ya kuanzishwa kwake
ikiwa ni pamoja na kukuza ufanisi na kiwango cha ufaulu katika Wilaya hiyo.
Katika kikao hicho
wadau wamechangia jumla ya shilingi milioni 3,900,000 ikiwa ni ahadi, Mifuko
100 ya saruji na rasilimali hamasa kwa vijana wa waliohitimu masomo ya sayansi
katika vyuo mbalimbali nchini watakaojitolea kufundisha katika shule zenye
upungufu wa walimu sayansi katika Wilaya ya Ikungi.
Mhe Mtaturu amewaeleza
washiriki wa kikao hicho namna ambavyo Uongozi wa Wilaya umejipanga kwa
kuhusisha michango ya wadau na nguvu za wananchi kwa ujumla kwa kuchangia
rasilimali fedha ama viwezeshi kama vile saruji, mchanga, kokoto na vitu vifaa
vingine vya ujenzi.
Akizungumza katika
kikao hicho kilichofanyika Lamada Hotel Jijini Dar es salaam akiwa ameambatana
na Mwalimu Athumani Salum ambaye ni Afisa elimu Sekondari wa Wilaya ya Ikungi, Mhe
Mtaturu alisema kuwa zipo changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu
Wilayani Ikungi ikiwa ni pamoja na Upungufu wa nyumba za walimu, Vyumba vya
madarasa, Ofisi za walimu, Maabara, Thamani mbalimbali, Matundu ya vyoo vya
walimu na wanafunzi.
Mhe Mtaturu
aliwaeleza wadau hao wa Mfuko wa elimu kuwa Wazo la kuanzisha Mfuko wa Elimu
lilitokana na kikao cha wadau wa elimu alichokiitisha mwezi Disemba, 2016 na
kubaini changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ikiwemo kushuka kwa ufaulu wa
wanafunzi kuanzia elimu ya msingi mpaka Sekondari.
Alisema Kikao
hicho kuliadhimiwa maazimio 43 ambayo yalizaa wazo la kuanzisha mfuko wa elimu
ambapo wazo hilo lilifikishwa kwenye baraza la madiwani na kupokelewa kwa kauli
moja ndipo mwezi Aprili mwaka 2017 baraza liliridhia kuanzishwa mfuko na kuteua
wajumbe 15 wa bodi ya mfuko wa elimu wa Wilaya ya Ikungi.
Mhe Mtaturu
alisema kuwa ili kukabiliana na changamoto zote hizo Bodi ilibainisha
kuhitajika jumla ya fedha taslimu shilingi bilioni 28.
Hata hivyo Baada
ya vikao mbalimbali vya maamuzi Bodi ya mfuko wa elimu imebainisha mpango
mkakati wa miaka mitatu kwa mtazamo wa Shule zenye hali mbaya zaidi hivyo
kuandaa makadirio ya gharama za shilingi Bilioni 3.
Mhe Mtaturu
alisema kuwa ili kufanikisha mpango huu kwa wakati husika Bodi ilitoa
mapendekezo ya wadau watakoombwa kuchangia mfuko ikiwemo Halmashauri ya Wilaya
ya Ikungi kuchangia 3% ya mapato yake ya ndani.
Sambamba na hayo pia
alielezea mikakati mbalimbali katika sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na kilimo
ambapo alisema wananchi wengi wanafanya kilimo cha kujikimu badala ya kilimo
cha biashara hivyo ili kukuza ufanisi wa pato la mkulima Uongozi wa Wilaya ya
Ikungi umekusudia kutatoa miche ya mbegu za korosho 500,000 bure kwani ni zao
rahisi kulima lisilohitaji uangalizi wa muda mrefu.
Alieza pia namna Wilaya
hiyo ilivyojipanga katika sekta ya Afya, Miundombinu, Sekta ya Maji, na
kuimarisha hali ya usalama ili wananchi kufanya kazi zao kwa ufasaha pasina
wasiwasi wowote.
Kwa upande wa wadau wa
elimu Wilaya ya Ikungi walimpongeza Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji
Jumanne Mtaturu kwa kuanzisha mfuko wa elimu wa Wilaya pamoja na kuwashirikisha
namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali wilayani humo.
Wamemuhakikishia kuwa
watatoa ushirikiano wa hali na mali ili kuinua sekta ya elimu na kuchagiza
ufanisi wa kukuza maendeleo katika Wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla wake.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
Mdau wa Mfuko wa elimu Wilaya ya Ikungi ambaye pia ni Afisa elimu Mkoa wa Dar es salam Mwalimu Khamis Lissu akichangia namna ya kuboresha elimu wilaya ya Ikungi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
Wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu katika Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisalimiana na Mzee Mjengi Gwau wakati wa kikao cha Wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani katika, Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017 katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam.
Mdau wa Mfuko wa elimu Wilaya ya Ikungi Ndg Nkrumah Munjori akichangi namna ya kuboresha elimu wilaya ya Ikungi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
Wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu katika Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi Alhaji Salumu M. Chima Akielezea hatua zilizofikiwa na kamati ya Mfuko wa elimu Wilaya ya Ikungi na wadau wa mfuko huo waishio Dar es salaam
Mdau wa Mfuko wa elimu Wilaya ya Ikungi Mzee Mjengi Gwau akichangia namna ya kuboresha elimu wilaya ya Ikungi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
Mdau wa Mfuko wa elimu Wilaya ya Ikungi ambaye pia ni Afisa elimu Mkoa wa Dar es salam Mwalimu Khamis Lissu akifatilia kwa makini kikao na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
Mdau wa Mfuko wa elimu Wilaya ya Ikungi Bi Khadija Kiimu akichangia namna ya kuboresha elimu wilaya ya Ikungi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
Mdau wa Mfuko wa elimu Wilaya ya Ikungi Ndg Omary Gwati akichangia namna ya kuboresha elimu wilaya ya Ikungi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
Mdau wa Mfuko wa elimu Wilaya ya Ikungi Ndg Josephat Bulali akichangia namna ya kuboresha elimu wilaya ya Ikungi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
0 comments:
Post a Comment