Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako akizindua
mabweni mawili katika Shule ya Sekondari Nasibugani iliyopo Wilaya ya
Mkuranga.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako akipanda mti katika shule ya Sekondari Nasibugani.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako akizindua
mabweni mawili yaliyokamilika katika shule sekondari Mwinyi iliyopo
Wilaya ya Mkuranga.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga akizungumza wananchi na wanafunzi katika shule ya Sekondari Nasibugani.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga, Mshamu Munde akizungumza wananchi na wanafunzi katika shule ya Sekondari Nasibugani.
Sehemu ya mabweni na nyumba za walimu ambazo zimefikia hatua ya boma
Sehemu ya mabweni na nyumba za walimu ambazo zimefikia hatua ya boma
Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii
SERIKALI
inatoa sh. bilioni 18.77 kwa ajili ya kugharamia elimu bure ili kila
mtanzania apate elimu bora na faida yake kwa serikali hiyo ni kuona
wanafunzi wanafaulu darasa la Saba na Kidato cha Nne na kuendelea na
elimu ya kidato cha tano na hadi chuo kikuu.
Hayo
ameyasema leo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce
Ndalichako wakati wa uzinduzi mabweni katika shule ya sekondari
Nasibugani ambayo ujenzi wake uko katika hatua ya mwisho pamoja na Shule
ya Sekondari Mwinyi ambayo ujenzi umekamilika kwa kuingia wanafunzi
katika mabweni hayo wilayani Mkuranga mkoani Pwani .
Profesa
Ndalichako amesema serikali ya awamu ya tano imeondoa imeondoa gharama
katika shule ya msingi na sekondari ili kuondosha mzigo kwa wazazi
wengine ambao walikuwa wanashindwa kugharamia elimu hiyo.
Amesema
mabweni katika shule ya sekondari Nasibugani na Mwinyi zenye Kidato cha
Kwanza hadi Sita ni kuongeza sehemu ya kumwezesha mwanafunzi kusoma kwa
muda mrefu na kuweza kondokana na vishawishi vinavyopatikana mtaani.
Aidha
amesema kuwa serikali itaendelea kuboresha shule mbalimbali ikiwemo
pamoja na makazi ya walimu yaliyo bora pamoja na huduma zingine ikwemo
umeme katika shule ya Sekondari Nasibugani.
Amesema
kuwa Mkuranga iko nyuma kielimu ni ukweli usiofichika hivyo walimu
pamoja na watendaji kuhimiza suala la elimu ili viwanda vilivyopo na
wanamkuranga wanufaike na sekta hiyo.
Waziri
Profesa Ndalichako amempongeza Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega
kuanzisha Program kwa wanafunzi wa sekondari kuwa Hakuna Kufeli.
Amesema
Program hiyo ifanywe kwa vitendo kwa wanafunzi kujitoa zaidi kusoma
kwani mtihani uko karibu lakini wakitumia program hiyo watafanya vizuri
na kuondoa sifuri katika shule zao na kuanza daraja la kwanza hadi la
tatu.
Nae
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga amesema kuwa wanaomba chuo
cha Ufundi katika wilaya hiyo ili vijana waweze kujiunga na kuweza
kutumika katika sekta ya viwanda vilivyojengwa Mkuranga.
Amesema
kuwa zaidi ya vijana 900 hawana ajira hivyo chuo cha ufundi ni sehemu
sahihi kwa vijana na wataendelea kuongeza mwaka hadi mwaka kadiri
wnavyohitimu.
Mbunge
wa Mkuranga Abdallah Ulega amesema kuwa jitihada mbalimbali katika
kuboresha miundombinu ya shule pamoja na serikali kuongeza walimu.Amesema kuwa wanafunzi wanavyofanya vizuri ni furaha na kuweza kuwa nguvu ya uandaji wa vijana katika mapinduzi ya elimu.
0 comments:
Post a Comment