Ofisa Mtendaji wa Kata ya Yombo iliyopo
Bagamoyo mkoani Pwani, Salimu Juma Mavaga (kushoto), akizungumza wakati
wa kupokea vizimbuzi 'ving'amuzi' vya Kampuni ya StarTimes vilivyo
tolewa kwa gharama ya sh,50,000 kwa wananchi wa vijiji vitatu vya
Yombo, Chasimba na Maimbwa wilayani humo jana.
Bibi Maendeleo ya Ustawi wa Jamii wa
Kata hiyo, Melitha Kiwanga akizungumza katika mkutano huo wakati
akiishukuru kampuni ya StarTimes kuwapelekea vizimbuzi hivyo.
Meneja Mauzo wa StarTimes, Tanzania,
Tang Jing Yu akizungumza katika mkutano huo kuhusu ugawaji wa vizimbuzi
hivyo na nia ya Rais wa China ya kusaidia nchi za Afrika katika mfumo wa
mawasiliano wa Kidigitali.
Meneja Masoko wa StarTimes, Yan Jing
Jing (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Ofisa wa Idara
ya Masoko wa kampuni hiyo, Furaha Mayala.
Mgeni rasmi katika shughuli hiyo Ofisa
Tarafa ya Yombo, Rashidi Kiwamba, akizungumza kwenye mkutano huo wakati
akiishukuru kampuni hiyo kwa kuwapelekea vizimbuzi hivyo kwa bei nafuu.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wakisubiri kulipia vizimbuzi hivyo na kwenda kufungiwa.
Wakina mama wakisubiri kulipia vizimbuzi hivyo.
Mgeni
rasmi katika shughuli hiyo Ofisa Tarafa ya Yombo, Rashidi Kiwamba
(kushoto), akimshukuru Meneja Mauzo wa StarTimes, Tang Jing Yu kwa
kuwapelekea huduma hiyo ya vizimbuzi katika karafa yao.
Mwalimu Hilda Stambuli wa Shule ya Msingi ya Yombo akishukuru kwa niaba ya wenzake kwa kupelekewa vizimbuzi hivyo kwa bei nafuu.
Meneja Mauzo wa StarTimes Tanzania, Tang
Jing Yu (wa tatu kushoto), akimkabidhi Mkazi wa Kijiji cha Matimbwa,
Shaabud Abdallah (wa pili kulia), Kizimbuzi na Dishi lake baada ya
kulipia sh.50,000 katika hafla iliyofanyika Kata ya Yombo wilayani
Bagamoyo mkoani Pwani jana. Wengine wanaoshuhudia kutoka kulia ni Meneja
Masoko wa StarTimes, Yan Jing Jing, Ofisa Tarafa ya Yombo, Rashid
Kiwamba, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Yombo, Salimu Juma Mavaga na Fundi
Mkuu wa StarTimes Michael Mkufya.
Ofisa Tarafa ya
Yombo, Rashid Kiwamba (katikati), akimkabidhi Kizimbuzi Mkazi wa Kata ya
Yombo, Ramadhan Kibwana Shomari (wa pili kulia), baada ya kukilipia.
Wengine kutoka kulia ni Ofisa Idara ya Masoko wa StarTimes, Furaha
Mayala, Meneja Masoko wa StarTimes, Yan Jing Jing, Ofisa Mtendaji wa
Kata ya Yombo, Salimu Mavaga, Meneja Mauzo Tang Jing Yu na Fundi Mkuu wa
StarTimes, Michael Mkufya.
Ofisa Tarafa ya
Yombo, Rashid Kiwamba (katikati), akimkabidhi Kizimbuzi Mkazi wa Kijiji
cha Chasimba,Miraj Mukadase (wa pili kulia), baada ya kukilipia. Wengine
kutoka kulia ni Ofisa Idara ya Masoko wa StarTimes, Furaha Mayala,
Meneja Masoko wa StarTimes, Yan Jing Jing, Ofisa Mtendaji wa Kata ya
Yombo, Salimu Mavaga, Meneja Mauzo Tang Jing Yu na Fundi Mkuu wa
StarTimes, Michael Mkufya.
Mkazi wa Kijiji cha Matimbwa, Shaabud Abdallah
akisaini fomu za malipo kabla ya kukabidhiwa kizimbuzi chake pamoja na
Dish. Kulia ni Ofisa Idara ya Mauzo wa StarTimes, Joanna Nuhu.
Wananchi wakisubiri kulipia vizambuzi kabla ya kwenda kufungiwa.
Walimu wa Shule ya Msingi ya Yombo wakiwa na madishi yao wakienda kufungiwa baada ya kulipia.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Vizimbuzi ya StarTimes
Tanzania imetoa vizimbuzi 50 kwa bei ya sh.50,000 kwa vijiji vitatu vya
Matimbwa, Chasimba na Yombo vilivyopo Bagamoyo mkoani Pwani.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya
kukabidhi vizimbuzi hivyo kwa wananchi wa vijiji hivyo, Meneja Mauzo wa
Kampuni hiyo Tang Jing Yu alisema lengo lao kubwa ni kusogeza huduma ya
kidigitali kwa wananchi.
"Kampuni yetu imejipanga kuhakikisha
inasaidia watu wa vijijini kupata huduma nzuri na kuwanufaisha katika
mfumo wa kidigitali" alisema Jing Yu.
Jing Yu alisema kwa awamu ya kwanza
wameanza kwa kusambaza vizimbuzi 50 chini ya mradi huo katika vijiji
hivyo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais wao wa China za kusaidia
nchi za Afrika kidigitali hasa katika maeneo ya vijijini.
Alisema China inajisikia fahari kubwa
kuona wananchi wa Afrika wananufaika na mradi huo na kwa hapa Tanzania
wameanza katika eneo hilo la Bagamoyo lakini lengo likiwa ni kuvifikia
vijiji vingi zaidi.
Ofisa Idara ya Masoko wa StarTimes,
Furaha Mayala alisema kabla ya kuanza mradi huo waliwatembea wananchi na
kuzungumza nao na kujionea changamoto kubwa ya kukosa mawasiliano hayo
ya kidigitali.
Alisema kampuni hiyo imetoa vizimbuzi
hivyo kwa watu 50 wa vijiji hivyo ambapo watatumia kwa kipindi cha mwezi
mmoja bila ya kulipia na amewataka wananchi wengine kuchangamkia fursa
hiyo.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Ofisa
Tarafa ya Yombo Rashid Kiwamba alisema kupelekewa vizimbuzi hivyo kwa
bei nafuu ni fursa kwao hasa katika kipindi hiki cha sayansi na
teknolojia ambapo dunia imekuwa ni kijiji kimoja.
Kiwamba alisema kwamba mradi huo
uliopelekwa na StarTimes ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dk.John
Magufuli aliyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu za kuhahikisha
huduma mbalimbali zinawafikia wananchi ikiwa ni pamoja na mawasiliano.
"Mradi huu tulioletewa na hawa ndugu
zetu wa StarTimes ni mzuri na ni mwanzo mzuri na mambo mengi mazuri
yanakuja hapa kwetu Yombo ni muhimu wananchi kuuchangamkia" alisema
Kawamba.
Mkazi wa Kijiji cha Chasimba Miraj
Mukadase aliishukuru kampuni hiyo kwa kuwapelekea mradi huo ambao
utawasaidia kupata taarifa mbalimbali kwa wakati.
"Tulikuwa tukikosa taarifa mbalimbali
kwa kuwa tulishindwa kupata vizimbuzi vya bei nafuu na vilivyobora
ambapo vilikuwa vikuzwa hadi sh.120, 000 lakini leo hii StarTimes
wametukomboa tunawapongeza sana" alisema Mukadase.
0 comments:
Post a Comment