Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mgombea
ubunge wa jimbo la kibaha mjini kupitia chama cha mapinduzi (CCM)
Silvestry Koka akiwahutubia wananchi wa kata ya picha ya ndege katika
moja ya mkikutano yake ya hadhara.
(Picha na Victor Masangu)
Mwenyekiti
wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Maulid Bundala
kushoto akimnadi mgombea huyo ubunge wa jimbo la Kibaha Silvestry koka
katika mkutano huo uliofanyika katika kata ya picha ya ndege.
……………………………………………………………………..
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
KATIKA
kuunga juhudi za serikali kuboresha miundombinu ya upataikanaji wa maji
Mgombea ubunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvessty Koka amesema kwamba
endapo akipata nasafi ya kuchaguliwa atahakikisha anasogeza huduma ya
maji katika kila mtaa lengo ikiwa ni kupunguza kero ya upatikanaji wa
maji kwa wananchi wake.
Koka
ameyasema hayo wakati wa mikutano yake ya hadhara ya kampeni kwa
wananchi wa mtaa wa mikongoro iliyopo kata ya Miswe pamoja na waanchi wa
mtaa wa zegeleni kata ya Visiga ambapo amesema anatambua usumbufu
wanaoupata wananchi wake hivyo suala hilo atalitafutia ufumbuzi wa
kudumu.
Mgombea
huyo alisema kwamba kwa sasa juhudi zake za kutandaza mabomba makubwa
katika jimbo la Kibaha mjini zimeshaanza kuzaa matunda hivyo ana imani
endapo mradi huo mkubwa pindi ukikamilika utaweza kuleta mabadiliko
makubwa na kuwasaidia wananchi ambao walikuwa wanakabiliwa na changamoto
ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji inamalizika.
“Ndugu
zangu wananchi adha ya upatikanaji wa maji kwa wananchi wa jimbo langi
hilo ninalitambua na wakati nipo madarakani nimlishaanza kufanya
mchakato wa kuomba mradi kwa serikali na nilikubaliwa na kwa sasa kuna
baadhi ya maeneo wameshaanza kunufaikamkupaata maji safiu na salama, na
hili ndilo lengo langu kubwa kwa ajili ya kuwakomboa wananchi wangu wa
kibaha,”.alisema Koka.
Pia
aliongeza kuwa huduma ya maji ni jambo la msingi sana kwa maisha ya
binadamu hivyo wanachi wa jimbo la kibaha na maeneo mengine wataweza
kunufaika na mradi huo ambao hawatapata tena shida kwani maji yatakuwa
yanawafikia katika mitaaa yao bila ya kuwa na usumbufu wowote kama
ilivyokuwa hapo awali.
Alifafanua
kuwa katika kipindi cha nyuma wananachi wake walikuwa wanateseka sana
kupata huduma ya maji safi na salama lakini kwa kipindi hiki cha miaka
mitano ilyopita kuna mabadiliko makubwa katika sekta hiyo kwani kuna
miradi mingin ya maji amabyo imefanyika na mingine badi inaendelea
kufanyika ili kuweza kutekeleza ilani ya chama ya kuboresha huduma ya
maji kwa wananchi.
Pia
ambali na hilo Koka akusita kuwaeleza wananchi wake wanatakiwa kuwa
makini kuakikisha wanailinda miradi yote ya maji sambamba na miundombinu
yake kwani imetumia gharama kubwa katika utekelezaji wake hivyo kila
mwananchi inapaswa awe mlinzi wa mwenzake.
Akizungumzia
suala la watendaji ambao watahujumu miundombinu pamoja na miradi hiyo
ya maji ambayo imeanzishwa kwa ajili ya kuweza kuwasaidia wananachi wa
jimbo la kibaha mjini kuondokana na kero ya upatikanani wa maji amedai
haweza kuwavulilia hata kidog na badala yake atawacukulia hatua kai z
akisheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
Kwa
upande wao wananchi wanaishi katika kata ya visiga pamoja na miswe
ambao hawakutaka majina yao yatajwe walisema kwamba mgombea huyo
anaetetea kiti chake katika kipindi chake ameweza kujitahidi
kushirikiana bega kwa bega katika kuleta mabadiliko katika kila sekta
japo kuna baahi ya watendaji wake ndio wanamwangusha kutokana na kuwa na
uroho wa madaraka.
0 comments:
Post a Comment