Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Ni siku kadhaa zimebakia kabla ya shindano la mama shujaa wa chakula linaloendeshwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow yenye kauli mbiu ya Wekeza kwa wakulima wadogo wadogo wanawake inalipa linaelekea ukingoni hiki kikiwa kipindi cha 18 ambapo wakina mama Shujaa wa Chakula walikuwa na mazoezi manne magumu ambayo kwa pamoja yaliitwa zoezi la kufa na kupona
Msanii Maarufu wa Bongo Movie ambaye pia ni Balozi wa Oxfam kupitia Kampeni ya Grow JB alikuwa ndiye msema chochote katika Zoezi hilo la aina yake.
Zoezi hilo lilifanyikia katika nyumba moja kijijini Kisanga ambayo ilikuwa haijaisha ambao Washiriki walitakiwa kufanya mambo Manne.
Ungana hapa nasi kutazama mazoezi hayo kwa umakini....
Balozi wa Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow ambaye pia ni Msanii maarufu wa Bongo Movie hapa Tanzania JB , akiwa ameanza na Hili zoezi la kwanza la kufungwa kitambaa cheusi ambapo baada ya kufungwa kitambaa hicho mshiriki alitakiwa kutafuta Bahasha tatu ambazo zipo katika Chumba cha kwanza ndani ya nyumba hiyo na baada ya kuzipata azifungue kisha atakutana na maswali ya Mabadiliko ya Tabia Nchi na Kilimo kwa Ujumla , akipata Jibu anaendelea na sehemu ya Pili.
Mshiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula Kushoto akipata maelekezo
Ndani ya Dakika Moja Mshiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula alitakiwa kufungua kamba kisha kueleza kwa mtazamo wake mwenyewe kwa kujibu swali juu ya unyanyasaji wa kijinsia, Hili lilikuwa ni zoezi la pili
Katika Chumba cha tatu kilikuwa na afadhali kidogo ambapo mshiriki alitakiwa kwenda katika chumba cha tatu na kukutana na matunda aina mengi mengi, kazi yake ilikuwa moja tuu kuchagua Tunda moja kisha kwenda Sebuleni na kulisema huyu alichagua Karoti
Akisoma karatasi
Kama haujawahi kuona ndio uone sasa watu wanalima katika cement.. hili lilikuwa zoezi la kufurahisha sana ambapo Ukilima katika Cement wewe si Mkulima ukiacha bila kulima wewe ni Mshindi... je unazani mama alifanyaje?
Mambo yanaendelea
0 comments:
Post a Comment