Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mtangaza nia ya Ubunge Jimbo la Bagamoyo, Mathew
Juma Salum Yangwe.
Mtangaza nia ya Ubunge Jimbo la Bagamoyo, Mathew
Juma
Salum Yangwe (katikati), akizungumza na makada na wanahabari wakati
akitangaza nia mjini Bagamoyo mkoani Pwani Pwani jana. Kushoto ni Meneja
wa Kampeni wa Mtangaza nia huyo, James Mbuligwe na Katibu wa Sera na
Mipango wa Mtangania huyo, Paul Kassanga.
Meneja wa Kampeni wa Mtangaza nia huyo, James Mbuligwe (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Katibu wa Sera na Mipango wa Mtangania huyo, Paul Kassanga(kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
Mzee Abdallah Ngumbe akizungumza katika mkutano huo na wakati akimpa ushauri mbalimbali mtangaza nia huyo.
Profesa Sameheni Kejeli akizungumza katika mkutano huo.
Mzee Hussein Lugome akizungumza katika mkutano huo.
Mama mzazi wa mtangania huyo, Mary Yungwe akiwasalimia makada wa CCM katika mkutano huo.
Mtangaza nia huyo akipongezwa na vijana baada ya mkutano huo.
Pongezi zikiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Makada wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo.
Mtangazania huyo akiwa na wadau wake.
Na Dotto Mwaibale
MBUNGE
wa Jimbo la Bagamoyo ambaye pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa amepata mpinzani baada ya kijana mdogo
kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mathew Yungwe kutangaza nia ya ubunge
katika jimbo hilo.
Akizungumza
na makada wa CCM na waaandishi wa habari mjini Bagamoyo mkoani Pwani
jana, Yungwe alisema ameamua kugombea nafasi hiyo ili kusukuma maendeleo
ya jimbo hilo ambayo yamekwama kwa muda mrefu.
"Wanaccm
wenzangu na wazee wangu nimeamua kugombea nafasi hii ili niwatumikie
kwani Bagamoyo naelewa vizuri na nitaendelea kuwa wilayani hapa ili
tushirikiane katika mambo mbalimbali ya nmaendeleo" alisema Yungwe.
Yungwe
alisema mambo atakayoyapa kipaumbele ni matatu, uchumi, Afya na
Mawasiliano na kuwa hata penda aitwe mbunge bali aitwe mratibu na kuwa
atakuwa na ofisi yake ya ubunge katika wilaya hiyo kwa lengo la kuwa
jirani na wananchi zaidi.
Alisema
maeneo mengine atakayoyafanyia kazi kwa kushirikiana na wananchi ni
pamoja na kuinua uchumi wa jimbo hilo kupitia uvuvi, kuweka mipango
mizuri ya kukusanya fedha kupitia viwanja vya michezo, utalii na mapato
yatokanayo na uwekezaji na ujenzi wa soko la kisasa.
Alisema
pia atashughulikia migogoro ya ardhi katika maeneo yote ya jimbo hilo
yakiwemo ya Zinga na Pande ambayo inapunguza kasi ya maendeleo ya
wananchi katika jimbo hilo.
Yungwe alisema kauli mbiu yake ni "Fikiri Tofauti, Badilika kwa Maendeleo Endelevu ya Bagamoyo.
Jimbo
la Bagamoyo katika kpindi cha miaka 10 tangu mwaka 2005 hadi sasa
lilikuwa likiongozwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk.
Shukuru Kawambwa. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
0 comments:
Post a Comment