Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAKAZI wa Mailimoja Wilaya ya Kibaha, Pwani wametakiwa kushiriki shughuli za maendeleo katika maeneo yao badala ya kusubiri kila jambo kuhamasishwa na viongozi wao.
Wito huo ulitolewa na Mwenyekiti wa Kibaha Mjini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mohamed Omari wakati akizungumza na Tanzania Daima baada ya ukarabati wa bomba la maji la shule ya msingi Mamlaka, wilayani hapa.
Omari alisema bomba hilo limekaa zaidi ya miezi minne bila kukarabatiwa baada ya kuharibika, hivyo uongozi wa shule kulazimika kununua maji nje ya shule wakati shule yao ina maji.
Akizungumzia hilo Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (Bavicha), Fadhili Ngonyani alisema kila siku wanafunzi walikuwa wakinunua zaidi ya ndoo moja ya maji ya kunywa jambo ambalo kama wananchi wangeshirikiana, wangetatua adha hiyo bila kuwategemea viongozi ambao hawakutilia mkazo suala hilo.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Joyce Kilango alikiri kwa njia ya simu kwamba viongozi wa chama hicho walifanya ukarabati wa bomba la shule lilisababisha ukosefu wa maji ya kunywa shuleni hapo na kulazimika kutumia sh 2,000 kwa siku kwa ajili ya maji ya kunywa ya wanafunzi kwa miezi minne mfululizo.
Baada ya kukamilika kwa ukarabati huo, Kilango alisema kwa sasa shule hiyo inkabiliwa na changamoto ya vyoo kwani vilivyopo havifai kwa matumizi.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment