Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MBUNGE wa Kisarawe Mkoa wa Pwani, Selemani Jafo amewataka wananchi
kushiriki katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yao
ili ikamilike kwa wakati badala ya kuiachia serikali pekee.
Akizungumza na wakazi wa kitongoji cha Masimba kata ya Mafizi juzi,
Jafo alisema huu si wakati wa kusubiri kufanyiwa, ni wakati wa kuonesha
ushirikiano kwa vitendo kwenye miradi inayotekelezwa katika maeneo
yao.
Alitoa kauli hiyo baada ya mpango wa kujenga nyumba ya mwalimu wa
shule ya msingi Masimbani kukwama kwa zaidi ya miezi sita kutokana na
wakandarasi kuhitaji fedha kubwa tofauti na iliyotolewa na halmashauri.
Mbunge huyo alisema, hakuna haja ya kuendelea kutafuta wakandarasi
kwani wote waliojitokeza wanahitaji zaidi ya sh milioni 28 hivyo ni
jukumu la wananchi kujipanga kwa zamu kuwasaidia wajenzi.
Jafo alimtaka Ofisa Elimu ya Msingi wilaya ya Kisarawe, Mohmed
Kahundi kuhakikisha anashirikiana na mhandisi wa wilaya na kuijenga
nyumba hiyo katika kipindi cha siku 45.
Nyumba hiyo ya mwalimu wa shule ya msingi Masimba itakapokamilika
itapunguza mrundikano wa walimu watano na familia zao katika nyumba
moja.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment