Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
JESHI
la Polisi Wilaya ya kipolisi Chalinze mkoani Pwani, linafanya kazi zake
kwenye kontena mali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na ufinyu wa
majengo ya ofisi.
Hayo yalisemwa mjini Chalinze jana na Diwani wa Bwilingu, Nasa Karama
wakati wa makabidhiano ya kompyuta na sh milioni 11 za kusaidia ujenzi
wa vituo vya polisi msaada uliotolewa na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani
Kikwete.
Karama alimueleza mbunge huyo kuwa tangu kituo hicho cha polisi
kipandishwe hadhi kuwa cha wilaya, shughuli zimeongezeka hali
iliyoilazimu CCM kuruhusu kontena lake litumike kama sehemu ya ofisi za
kituo hicho.
Alisema askari wa kituo hicho hawana nyumba za kuishi, wamepanga
uraiani hivyo alimuomba Ridhiwani kusaidia ujenzi wa nyumba za askari
polisi hao.
Akikabidhi misaada hiyo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich
Matei mbunge huyo alisema kompyuta na mashine ya kudurufu nyaraka
zitasaidia kuhifadhi kumbukumbu na kuacha matumizi ya steshenari za nje
ya ofisi.
Akishukuru baada ya kukabidhiwa misaada hiyo, Kamanda Matei alisema
kituo cha Chalinze kimepandishwa hadhi ni kipya hivyo kinahitaji
maboresho.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment