Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Pilika pilika za hapa na pale
zilionekana katika kijiji cha Maisha Plus ambapo wanakijiji walionekana
wakishughulisha na shughuli binafsi za kifamilia, kubadilishana mawazo na
uzoefu walionao
Wanakijiji wa Kijiji cha Maisha Plus wakifuatilia Mada kwa makini wakati ikiwasilishwa na TGNP
Pia waliweza kupata darasa kutoka kwa wawezeshaji wa masuala
ya kijinsia nchini wa Mtandao wa Jinsia Tanzania. Lengo la darasa hili ni
kuwawezesha washiriki wa Maisha Plus vijana na mama shujaa wa chakula kutambua
na kuelewa masuala ya kijinsia kwenye shughuli zao za kazi wanazozifanya kwani
washiriki wanatoka sehemu mbalimbali na wanajishughulisha na kazi tafauti
ambazo zinatofautiana wengine ni wasanii, waandishi wa habari, wafanyakazi wa
taasisi mbalimbali, wengine bado ni wanafunzi wanaendelea na masoma
Bakari Kharid aliyesimama Mshiriki wa Maisha Plus Kutoka Mkoa wa Shinyanga Nchini Tanzania akiwasilisha Mada
Tunajua
kwamba wakipata masuala muhimu ya kutetea usawa wa kijinsia na wanayaelewa huko
wanapofanya kazi zao baadaye watayatumia vizuri sana na wataweza kuleta
mabadiliko katika nchi yetu ndiyo maana tumeshiriki kwa pamoja kuhakikisha
kwamba tunawajengea uwezo kwenye kampeni ya ‘Haki
ya Kiuchumi: Rasilimali Ziwanufaishe Wanawake Walioko Pembezoni’ alisema
Deogratius Temba, Afisa Habari wa TGNP Mtandao.
Deogratius Temba kutoka TGNP akiwasilisha mada na kutoa mafunzo juu ya Jinsia
Aliendelea na kusema kuwa
tumefurahi sana kuwepo na mjadala huu mpana kupitia picha chokozi na kuona ni
fursa pekee kuendelea kusambaza kampeni ya Haki
ya Uchumi kwa jamii nzima mjini na huko vijijini kwasababu watu walio
vijijini ni wengi na watakapoenda kule
wataendeleza hii kampeni na lubadilisha jamii yetu ya kitanzania.
Mmoja wa Washiriki wa Mama Shujaa wa Chakula akitoa maoni wakati wa semina hiyo ya Jinsia katika Kijiji cha Maisha Plus
Suala la na mfumo dume na umiliki
wa ardhi limejitokeza wakatii wa majadiliano kwani mfumo dume na umiliki wa
uchumi vinashirikiana kwamba kama kuna mfumo dume mwanamke na kijana hawawezi
kumiliki uchumi hivyo kuendelea kubeba
mzigo mkuwa wa kulea familia.
Wanakijiji wakifuatilia Mjadala kwa umakini
Wanakijiji wa Maisha Plus
walifurahishwa na mjadala huu kwani una nia ya kumkomboa mwanamke kutokana na
yale majukumu mazito anayokuwanayo nyumbani na jamii nzima inayomzunguka na
kuwa na haki ya kumiliki ardhi na siyo kuwa mzalishaji pekee kama ilivyo sasa
katika jamii nyingi hapa nchini. Vile vile wameweza kuona umuhimu wa kuhudhuria
vikao vya kijiji ambapo wanaweza kupata fursa ya kutoa maoni na kushiriki moja
kwa moja katika mchakato wa bajeti ya serikali kupitia serikali ya mtaa ambapo
wengi wao hawakuwa na ufahamu huo.
Mama shujaa pia walitoa uzoefu
wao kuhusu nafasi ya mwanamke katika jamii wanazotoka na kusema kuwa umiliki wa
ardhi kwa kinamama bado ni changamoto kwani wengi wao wamebaki kuwa wazalishaji
tu na kutumia ile ardhi na siyo kumiliki jambo ambalo linarudisha nyuma juhudi
za kinamama katika kujikomboa kiuchumi. Vile vile walipongeza waandaaji kwa
kuwa na mpango wa kutoa mafunzo mbalimbali yatakayowasaidia washiriki katika
sehemu walizotoka na jamii kwa ujumla.
MAISHA PLUS/ MAMA SHUJAA WA CHAKULA
0 comments:
Post a Comment